KANUNI ZA KUFANIKIWA KUTOKA KATIKA UCHUMI MDOGO KWENDA UCHUMI MKUBWA
KANUNI ZA
KUFANIKIWA KUTOKA KATIKA UCHUMI MDOGO KWENDA UCHUMI MKUBWA
Utangulizi:
• Tunaishi
katika nyakati ambazo ili mtu aweze kuyamudu maisha vizuri, anahitaji kuwa na
vyanzo kadhaa vya kimapato na sio chanzo kimoja.
• Ujasiliamali ndio moja ya ndio kitu
kitakachoweza kuleta suluhisho la kiuchumi na kuboresha maisha ya mtu. •
Kuongeza kipato zaidi ya mshahara unao upata.
KANUNI ZA KUFANIKIWA KIUCHUMI 1. Mafanikio ya kiuchumi/kibiashara hayaanzii
kwenye kuwa na mtaji – bali maarifa ya biashara yenyewe.
• Kabla
hujatafuta mtaji wa biashara unayotaka kuifanya, tafuta kwanza maarifa ya juu
ya hiyo biashara unayotaka kuifanya.
• Mitaji ya
watu wengi imeteketea kwasababu walianza kutafuta mtaji wa biashara kabla ya
kutafuta maarifa juu ya biashara anayotaka kuifanya.
• Usichukue
taarifa za mtaani ukaenda kukopa mtaji uanze biashara. Mtaji utapotea na
utabaki kulipa deni la mtaji ambao haukufanikisha lengo – That is called a step
back. 2. Mafanikio ya kiuchumi/biashara yanategemea kiwango cha usimamizi wa
biashara au kitegeuchumi hicho.
• Ni nani
unayemuweka kusimamia hiyo biashara. i. Usitafute watu na kuwapa usimamizi wa
biashara kwa Misingi ya Undugu au Urafiki unless anao ujuzi na uwezo huo wa
jukumu hilo. ii. Usitafute watu na kuwapa usimamizi wa biashara kwa Misingi ya
Ukabila. iii. Usitafute watu na kuwapa kazi au majukumu kwa Misingi ya
Kumuhurumia Mtu.
✓ Kwao wazazi wake wote wamekufa
kwahiyo ngoja tu tumpe hii kazi hata kama hajasomea.
✓ Huyu ni mjane anamzigo mkubwa wa
watoto nyuma yake ngoja tu ajibanze hapa asogeze siku.
✓
Huyu alizalishwaga sana na wanaume wote wakamkimbia sasa ngoja tu tumpachike
hapa naye yeye apate pate chochote cha kumsaidia. 3. Mafanikio ya
kiuchumi/biashara yanahitaji Nidhamu ya Fedha na Matumizi. Note: Kinachofanya
watu wengi washindwe kufikia ndoto za mafanikio ya uchumi na maisha yao ni
tatizo la matumizi mabaya ya fedha yasiyo na nidhamu
. • Jifunze kuweka
akiba
✓
Fungua akaunti hata kama kipato chako ni kidogo.
✓
Usisubiri mpaka utakapokuwa tajiri ndio utaanza kuweka akiba.
✓ Usisubiri mpaka utakapokuwa umepata
vingi ndipo uanze kuweka akiba.
• Watu waliofanikiwa sana katika maisha ni
wale waliojitahidi kujinyima na kujijengea mazoea ya kuweka akiba kidogo
kidogo. (Accumulation)
• Ukipata pesa wekeza kwanza kisha kula
kinachobaki. Tofauti ya Masikini na Tajiri
✓
Masikini akipata pesa anakula kwanza kisha anawekeza kama itakuwa imebakia.
✓ Tajiri akipata pesa anawekeza kwanza
kisha anakula inayobaki.
• Epuka
kukopa kwa shughuli isiyo ya maendeleo.
✓ Jiepushe na kukopa kopa vitu kutoka
kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wanaokopesha vitu mbali mbali ambavyo sio
vya muhimu. ✓ Usikope kwajili ya harusi – tafuta
michango na ukipata kidogo fanya harusi ndogo kulingana na kipato chako usitake
mambo makuu yatakuumiza.
✓ Usikope kwajili ya sherehe kama
birthday, graduation nk.
✓ Ukikopa iwe ni kitu cha kimaendeleo.
• Jifunze
kuweka vipaumbele juu ya mahitaji muhimu utakayo fanya kwa pesa iliyopo mkononi
mwako.
✓ Usijaribu kutaka kutekeleza kila
hitaji.
✓ Mahitaji ni mengi hutaweza
kuyamaliza.
✓ Michango ni mingi hutaweza
kumchangia kila mtu.
✓ Madeni ni mengi hutaweza kuyalipa
yote kwa mara moja.
✓ Sio kila unacho kitaka ni lazima
ukipate.
✓ There is difference bebween what you
want and what you need. • Usikope vitu ambavyo vitakuwa vinakunyonya Zaidi
badala ya kukuingizia kipato.
✓ Mfano unakopa gari la kutembelea tu
ambalo sio la lazima na halikuingizii kitu na huna uwezo wa kulihudumia.
✓
Usikope gari huku huna uhakika wa mafuta au kulihudumia.
✓
Mahitaji ya gari ni kama mahitaji ya mwanadamu tu:
❖ Gari linahitaji kula na kunywa.
❖ Gari linahitaji kuoga.
❖ Gari linahitaji kwenda hospitali
mara kwa mara.
❖ Gari linahitaji kulipiwa kodi na
ushuru wa mara kwa mara. Kama unakipato kidogo na hujafanya mambo mengine ya
kipaumbele, usitangulize kukopa gari kwanza na hasa gari ambayo sio ya
kukuongezea kipato.
• Usipende kukaa na fedha mfukoni, nyumbani au
kwenye simu zako. Jitahidi uwe na akaunti yako na kila mara tupia huko chochote
kinachoingia. Mkononi ibaki pesa kidogo tu ya matumizi madogo madogo.
✓
Usipende kutembea na ATM card yako kila unapokwenda.
• Usimpe
pesa Rafiki yakow ala ndugu yako hata kama ni mzazi wako au kaka au dada
akuwekee ili siku ukiwa unazihitaji akupe. Pesa zako zitunze mwenyewe. Fungua
akauti yako fungia pesa zako huko.
✓ Mtaharibu Urafiki wenu,
✓ Mtaharibu undugu wenu. 4. Dhibiti
vyanzo vyako vya msongo wa mawazo
• Msongo wa mawazo unamchango mkubwa sana
katika kuudhohofisha uchumi wa mtu
. • Msongo
wa mawazo unapunguza uwezo wa mtu kufikiri kwa kina.
• Msongo wa mawazo unapunguza uwezo wa mtu wa
ubunifu.
• Msongo wa
mawazo unapunguza uwezo wa mtu katika kufanya maamuzi. How:
• Ishi kwa
kiwango chako
Social
involvement
• Let your
feelings out – Kucheka au Kulia.
• Kula
chakula kizuri pale inapowezekana.
• Lala
mahari Pazuri – Mahali unapolala pana uhusiano mkubwa sana na kiwango cha
Stres.
• Pata rafiki mzuri unayemwamini wa kumshirikisha mambo yako na hasa yale yanayo kuumiza usibaki nayo moyoni.