Dec 15, 2021

FAIDA 6 ZA KUWA NA WEBSITE KWA AJILI YA BIASHARA

 

Je umekua ukisikia tuu swala la kuwa na website lakini hujaelewa kwanini haswa uwe na website kwa ajili ya biashara au asasi yako isiyo ya kiserikali (NGO)? Au unayo website lakini haujaona bado faida za kuwa na website ? Basi makala hii itakupasha  faida haswa ya kuwa na website kwa namna ambayo pengine hujawahi kufikiria.



Hakuna wakati ambao website ni ya muhimu kama wakati ambapo tupo katika zama za utandawazi. Yawezekana ukajiona kuwa unachofanya ni kidogo hivyo hauhitaji website , hata hivyo kuna mengi utakua unakosa kwa kutokujikita katika kuwa na website kwa biashara au asasi yako.

 

Kukipa thamani ufanyacho

Imekua kawaida watu wengi kuamini kuwa biashara au asasi yenye website basi itakua makini . Hata hivyo sio tuu website ili mradi website. Unatakiwa uwe na website ambayo kweli inaonyesha umakini na ubora wa asasi au biashara yako hii inajumuisha website yenye muonekano mzuri, yenye maelezo yaliyokamilika, yenye taarifa ambazo kweli.

 

Kuleta ushawishi

Unahitaji website ili kuweza kujenga uaminifu na kuonekana kweli upo serious. Website yako itakupa nafasi ya kuwaeleza watu kwa umakini na kwa ushawishi kile unachofanya  na kwanini wakutafute wewe. Tena website itakusaidia kufanya ushawishi huu kwa watu wengi sana kuliko kuwa tuu na vipeperushi ambavyo utasambaza kwa watu wachache.

 

Kuelezea Ufanyacho

Website hukufanya uwe na nafasi ya kueleza mambo uyafanyacho kwa watu wengi zaidi. Ni kweli unaweza kuwa na akaunti nyingi za mitandao ya kijamii . Lakini watu wengi hawatopata kukufahamu vizuri kama sio kupitia kwa website yako ambapo utakua na kurasa zilizopangiliwa vema kabisa.

 

Kupatikana wakati masaa 24 siku 7 za wiki

Ofisi yako hufungwa , duka lako hufungwa, lakini website yaweza kupatikana masaa 24 siku 7 za wiki. Hivyo kuwa na website ni fursa kwako kuwafaikia walengwa wako masaa yote kila siku.

 

Kuwasiliana na kuwaelimisha wateja

Kwa kutumia blog itakayoambatana na website yako utaweza kuwapatia wateja wako na wale wateja watarajiwa Makala ambazo zitawaelimisha na kuwavuta karibu na wewe. Pia ni nafasi yako ya kuwapa updates kuhusu bidhaa mpya unazotaka kutoa au mabadiliko mengine ya kiutendaji , kimarketing na sera za biashara au asasi yako.

 

Kuwa na email address binafsi

Website itakufanya uweze kuwa na email address inayotaja jina la biashara yako. Haipendezi na haionekani kuwa “professional” pale unapohitajika kutaja email address yako halafu ukatumia email yenye domain ya makampuni makubwa kama gmail, yahoo au Hotmail. Kama kampuni yako ni ABC Limited, basi ni vema ukasema jinalako@abc.com au  jinalako@abc.co.tz

 

Kwa wewe unayetaka kuwa na website inayokunufaisha tuwasiliane kwa WhatsApp 0745507517tukusaidie. Au comment  kwa hii post.

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home